Jumapili 4 Oktoba 2026 - 22:59
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Laichapisha Barua kwa Wananchi wa Marekani; Larejelea Dhamira ya Pamoja ya Imam Mahdi (as) na Nabii Isa (as) + Video

Hawza/ Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran hivi karibuni limetoa barua ya kina iliyoelekezwa kwa wananchi wa Marekani, ambayo pamoja na kujadili masuala ya kisiasa na kijeshi, imeelekeza pia fikra kwenye baadhi ya itikadi zinazofanana kati ya Uislamu na Ukristo kuhusu matukio ya mwisho wa zama.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran hivi karibuni limetoa barua ya kina iliyoelekezwa kwa wananchi wa Marekani, ambayo pamoja na kujadili masuala ya kisiasa na kijeshi, imeelekeza pia fikra kwenye baadhi ya itikadi zinazofanana kati ya Uislamu na Ukristo kuhusu matukio ya zama za mwisho.

Katika barua hiyo ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, imeashiriwa kwamba katika kipindi cha kudhihiri Imam Mahdi (as), Nabii Isa Masih (as) atakuwa pamoja na Imam Mahdi (as), na kwamba waumini wa kweli watasimama pamoja katika kuasisi uadilifu na haki, na kukabiliana na dhuluma na ukandamizaji.

Miongoni mwa vipengele muhimu vya barua hiyo ni kutofautisha kati ya wananchi wa Marekani na viongozi wa kisiasa wanaoitawala nchi hiyo, kwa kuelekeza ujumbe wake moja kwa moja wananchi wa Marekani, barua hiyo imewataka kutafakari uchaguzi wao wa kihistoria na kuamua msimamo wao dhidi ya sura mbalimbali za dhuluma na utawala wa kimabavu.

Jambo hili linastahili kuzingatiwa zaidi kwa sababu katika miaka iliyopita, baadhi ya vuguvugu na makundi ya Kizayuni yenye misingi ya Kikristo nchini Marekani yamejaribu kuwasilisha mtazamo fulani kuhusu matukio ya mwisho wa zama, ambao ndani yake Imam Mahdi (as) anaoneshwa kuwa mpinzani wa Nabii Isa Masih (as).

Kinyume na mtazamo huo, ufafanuzi sahihi wa mitazamo inayofanana kati ya Uislamu na Ukristo kuhusu matukio ya mwisho wa zama unaweza kuweka wazi kwamba itikadi ya kuja Mwokozi aliyeahidiwa inaweza kuwa njia ya kuwaleta pamoja wafuasi wa kweli wa dini mbalimbali katika kupinga dhuluma, ukosefu wa haki na udikteta.

Katika muktadha huu, moja ya majukumu muhimu ya wanazuoni na wanaharakati wa kidini wanaojishughulisha na masuala ya Mahdawiyya ni kueleza kwa usahihi itikadi zinazofanana kati ya Uislamu na Ukristo, pamoja na kutekeleza wajibu wao katika kuzuia kuenezwa mitazamo potofu na iliyopotoshwa kuhusu Mwokozi aliyeahidiwa miongoni mwa wafuasi wa dini mbalimbali.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha